MKMkatabaHQ
Read in English Anza sasa
“Mali bila daftari hupotea bila habari.”

Jifunze kutumia daftari lako

Majibu mafupi kwa maswali ya kila siku — kisha bonyeza Fanya sasa kuendelea ndani ya MKHQ.

HQ au Tovuti kamili?Namba moja · Akaunti moja · Daftari moja · Weka HQ kwenye Home Screen
📱HQ — kwenye simuKila siku
  • 💬Andika unachojua — mazungumzo, sio fomu
  • Mpangaji, malipo, notisi — papo hapo
  • 👆Alama ya kidole baada ya usajili — hakuna OTP tena
  • 📶Inafanya kazi hata mtandao ukiwa dhaifu
🖥️Tovuti kamiliKazi kubwa
  • 📊Majedwali ya mikataba, ripoti, na uchambuzi
  • 👥Team, taarifa za biashara, mipangilio
  • Kila kilichopo HQ kipo hapa — na mengi zaidi
  • ✉️Unaingia kwa OTP kila mara
Huna uhakika uanzie wapi? Anza na HQ. Usajili ni mmoja, mtumiaji ni yule yule, nafasi (role) ni ile ile — na kila unachokiona HQ kipo pia kwenye tovuti.

📲 Weka HQ kwenye Home Screen

iPhone: fungua mkatabahq.com/hq kwenye Safari → kitufe cha Share → "Add to Home Screen".
Android: Chrome → menyu ⋮ → "Add to Home screen". Sasa HQ inafunguka kama app.

👆 Washa alama ya kidole (passkey)

Baada ya kuingia mara ya kwanza: Akaunti → "Washa passkey". Kuanzia hapo unafungua kwa kidole au uso — hakuna kusubiri OTP tena kwenye simu.

MalipoHQ & Tovuti Amana (deposit) inakaaje kwenye hesabu? Amana hurekodiwa siku ya mkataba lakini haigawiwi kwenye invoice mpaka wewe useme. Ni pesa iliyoshikiliwa — sio kodi iliyolipwa. Soma jibu → HQ — kwenye simuHQ · Simu App imekwama au haionyeshi taarifa mpya — nifanye nini? Vuta skrini chini (pull to refresh), au tumia "Refresh" kwenye menyu ya biashara yako. Mtandao ukiwa dhaifu, taarifa za mwisho zilizohifadhiwa zinaonekana kwanza. Soma jibu → WapangajiTovuti Bodi ya mikataba inaniambia nini — Overdue, Inaisha karibuni, Wazi? Ni ishara tatu, sio hali tatu. Overdue — mkataba hai wenye deni. Inaisha karibuni — mkataba hai unaokwisha ndani ya siku 60. Wazi — chumba kisicho na mkataba hai. Zinabadilika zenyewe kadri daftari linavyobadilika. Soma jibu → WapangajiHQ · Simu Kwa nini chumba kinaonyesha wazi wakati mpangaji yupo? Chumba huwa "wazi" pale mkataba unapokwisha kwenye daftari — hata kama mtu bado yupo ndani. Ongeza mkataba (renew) na kitarudi "kimejaa". Soma jibu → Kuanza & AkauntiTovuti Nimefungua app — kwa nini inanionyesha "Continue as"? MKHQ inakukumbuka — inahitaji tu uthibitishe ni wewe (OTP). Hupotezi chochote; taarifa zako zipo salama. Bonyeza jina lako na uendelee. Soma jibu → WapangajiHQ & Tovuti Daftari la PangoXray linafanyaje kazi — kwa picha moja? Mnyororo mmoja: chumba kinapangishwa kwa MKATABA; mkataba unazalisha invoice kila mzunguko wake (mwezi, miezi sita, mwaka); malipo yanakaa kwenye invoice; na ishara zote (deni, inaisha, wazi) zinajihesabu kutoka hapo. Ukishaushika mnyororo huu, kila kitu kingine kinajieleza. Soma jibu → Duka (ShopXray)Tovuti Drop-off ni nini tofauti na visit ya kawaida? Visit ya kawaida — mteja yupo, huduma inaisha, analipa. Drop-off — mteja anaacha kitu (nguo, simu, kiatu) na kurudi baadaye, hivyo jina na namba yake ni muhimu. Soma jibu → Duka (ShopXray)Tovuti Daftari la duka linafanyaje kazi — kwa picha moja? Mnyororo mmoja: siku inafunguliwa; kila mteja anapata VISIT yake; huduma na bidhaa zinaingia kama mistari yenye bei; malipo yanafunga visit; na mwisho wa siku, pesa zilizohesabiwa zinalinganishwa na daftari. Visit ndiyo kitovu — kila kitu kinazunguka hapo. Soma jibu → Tovuti kamiliTovuti Tovuti kamili inatofautianaje na HQ? HQ (simu) ni ya kazi za kila siku — haraka, mazungumzo. Tovuti kamili ni ya kazi kubwa — majedwali ya mikataba, ripoti, team, na taarifa za biashara. Taarifa ni zile zile — milango miwili, daftari moja. Soma jibu → HQ — kwenye simuHQ · Simu HQ ni nini — na vianzio (starters) vinafanyaje kazi? HQ ni daftari lako kwenye simu — mazungumzo, sio fomu. Vianzio ni vitufe vinavyotangaza unachotaka ("Mpangaji mpya", "Rekodi malipo") — kisha unaandika kwa maneno yako. Soma jibu → Duka (ShopXray)HQ · Simu Kazi kwenye HQ ni nini — duka linatumia lini simu, lini tovuti? Kazi ni duka lako mfukoni — siku ya leo inavyosimama, na risiti mkononi. Kaunta inaendeshwa kwenye tovuti (visits sambamba, kufunga siku); simu ni ya kuangalia na kufikisha: unaona hali ya leo popote ulipo, na "Tuma risiti" inampelekea mteja risiti kamili WhatsApp — kitufe kimoja. Soma jibu → HQ — kwenye simuHQ · Simu Nikigusa jina la biashara yangu, menyu ile ina nini? Kila kitu cha akaunti mahali pamoja: wewe (jina, barua pepe, pande za biashara), biashara zako (kubadilisha, taarifa zake kwa kalamu), bili yako ya MKHQ, Jifunze, na kutoka. Biashara zaidi ya moja? Zote humu — gusa moja kuhamia. Soma jibu → WapangajiHQ & Tovuti Mkataba wa pango unapatikanaje ukiwa tayari ku-share? Kila mkataba unaotengenezwa MKHQ unakuwa na kitufe cha "Share WhatsApp" — hati kamili, ukurasa mmoja, inasomeka kirahisi. Hakuna ku-download wala ku-print lazima. Soma jibu → WapangajiHQ & Tovuti Mkataba wa pango una vitu gani ndani? Mkataba unajengwa kutoka kumbukumbu zako — hauandiki mara mbili. Ndani yake kuna pande mbili (wewe na mpangaji), chumba, tarehe za kuanza na kuisha, kodi na mzunguko wake, amana, na masharti. Soma jibu → Kuanza & AkauntiHQ & Tovuti Naanzaje — akaunti na biashara yangu ya kwanza? Namba yako ya simu ndiyo akaunti yako — hakuna password ya kukariri. Unathibitisha kwa OTP, unaweka jina la biashara, na daftari lako lipo tayari. Soma jibu → MalipoHQ & Tovuti Nimepokea kodi — narekodi wapi? Kwenye chumba au mpangaji husika, tumia "Rekodi malipo". Malipo yanakaa kwenye invoice halisi — hivyo deni linalobaki huonekana kwa usahihi. Soma jibu → MalipoHQ & Tovuti Njia za malipo zinawekwa wapi — mpangaji ajue alipe vipi? Kwenye taarifa za biashara yako (biz profile) — sio kwenye kila mkataba. Unaweka njia zako mara moja (mf. Lipa Namba, akaunti ya benki), na zinasafiri na nyaraka zako: mpangaji anajua wapi pa kulipa bila kuuliza. Soma jibu → WapangajiHQ · Simu Namtumiaje mpangaji notisi ya ku-renew? Sema tu — "Mtumie Juma notice ya ku-renew mkataba wake." MKHQ inatumia kumbukumbu zilizopo; wewe unapitia na ku-share WhatsApp. Soma jibu → WapangajiHQ · Simu Mpangaji mpya ameingia — naanzia wapi? Huna haja ya kujua fomu gani. Andika tu unachojua kwenye HQ — jina, chumba, alicholipa, anaingia lini — na MKHQ itapanga mkataba tayari. Soma jibu → WapangajiHQ & Tovuti PangoXray ni ya nani — na inasimamia nini hasa? PangoXray ni daftari la mwenye nyumba — vyumba, wapangaji, mikataba, na kodi. Kitovu chake ni MKATABA: kila chumba, malipo, na notisi vinazunguka mkataba ulio hai. Soma jibu → HQ — kwenye simuHQ · Simu Portfolio kwenye HQ inanionyesha nini? Vyumba vyako vyote kwa mtazamo mmoja — kilichojaa, kilicho wazi, deni, na unachopoteza kwa mwezi vyumba vikiwa wazi. Kadi nyeusi juu ni jumla ya biashara nzima. Soma jibu → Duka (ShopXray)HQ & Tovuti ShopXray ni ya nani — si ni POS tu ya kuandika mauzo? Inaanza hivyo — visit ni kama noti ya haraka ya mauzo. Mpaka utakapogundua kwa nini si POS: huduma zinatumia vifaa vya duka visivyoonekana kwenye risiti (nywele zinatumia dawa, cherehani inatumia uzi), bei zinajipanga zenyewe kutoka orodha yako, na wateja kadhaa wanahudumiwa SAMBAMBA — kila mmoja na visit yake iliyo wazi. Soma jibu → Duka (ShopXray)Tovuti Kufungua na kufunga siku kuna maana gani? Siku ni ukurasa wa daftari. Kuifungua asubuhi kunaanzisha ukurasa mpya; kuifunga jioni kunauhitimisha — unahesabu cash na pesa za simu ulizonazo, na daftari linakuambia kama vinalingana na mauzo. Tofauti inaonekana PAPO HAPO, sio mwisho wa mwezi. Soma jibu → HQ — kwenye simuHQ · Simu Skrini ya HQ ina nini — kila kitu kinachoonekana? Vitu vinne tu. Juu: jina la biashara yako (gusa — menyu yako), kitabu (Jifunze), na SW/EN (badilisha lugha). Katikati: mazungumzo yako — daftari lenyewe. Chini: alama ya + inayoita vianzio. Hakuna zaidi — kila kingine kinakuja kwenye mazungumzo. Soma jibu → Kuanza & AkauntiTovuti Nawezaje kumwongeza msaidizi (team member)? Unamwalika kwa namba yake ya simu na kumpa nafasi (role) — anachoona na kufanya kinategemea nafasi hiyo. Wewe ndiye mmiliki daima. Soma jibu → Duka (ShopXray)Tovuti Kwa nini nisitumie jina kama "Walkin"? Visit inaweza kuwa bila mteja — hiyo ni sawa. Lakini ukiweka jina, liwe la mtu halisi. Risiti, WhatsApp, na madeni vinamtambua mtu — sio "Walkin 3". Soma jibu →